JIJI LA TANGA NA MKOA WAKE KWA UJUMLA MCHAWI WAKE NI NANI?
Ukiwa
hujawahi fika katika mji huu ukisikia stori zake unaweza kuvutika hasa
katika mpangilio wa barabara, suala la kusadikika la mapenzi, vyakula,
matunda kila haja, sasa hebu jaribu fika katika jiji hili na manispaa ya
kihistoria yenye mengi yaliovutia hapo kale.
Magofu ya viwanda
vilivyokufa ndio yataanza kukukaribisha, nyumba chakavu zenye kukatisha
tamaa, mji uliopoa kuashiria ni wa kale hasaa, wakazi wake wapo aina
mbili wapo wavivu hawa kila kazi kwao mbaya mida mingi maskani/ama
vijiweni wakipiga soga na wanatamani maisha mazuri hivyo wanaamini
katika kuzamia, na kuletewa ajira zenye ujira mkubwa mikononi, wapo
wakazi aina ya pili hawa ni wachakarikaji hasa na kila lazo kwao twende
tatizo uduni wa elimu walionao ila si kikwazo cha kufanikiwa katika
kipato na riziki.
Tatizo la Tanga halijawahi pata viongozi wakombozi
ambao watakuwa na uchungu na mji ambao wataweza kuwaongoza wananchi
kuwashawishi kuvuka na kupiga hatua hasa katika kutumia rasilimali zao,
hapa si madiwani na wabunge kutoka chama chochote toka enzi na kale, sio
viongozi wakuteuliwa, kama Mkurugenzi, RAC, DAC, DC wala RC, huoni
cheche katika mikakati thabiti kutumia rasilimali ziweze wanufaisha
wananchi. Lakini pia viongozi hawa wanatumia mianya ya wakazi kutokuhoji
kujinufaisha kimaslahi.
Tanga ni shamba la bibi, ni zaidi ya miaka
50 mandhari na taswira ya mji wa Tanga iko palepale imepoa wenyewe
wanasema mji unapiga (mark time) hauendi mbele upo upo tuu'! Tanga
katuroga nani?
Ukithubutu kufanya kitu na kikaonekana katika taswira
ya ukubwa basi jidhatiti haswa maana watatokea watakao hakikisha
hufanikiwi kwa hoja kwanini iwe wewe na si wao kufanya na hata ukiwapa
wafanye watafeli, yapo mengi ila nani mchawi Tanga? Wasomi na vijana
wanaongoza kuukimbia mji wao, matajiri na maarufu hawautaki asilani!
Tatizo nini Tanga?
No comments:
Post a Comment